Maswali na Majibu Muhimu kwa Ajira ya Afisa Mtendaji wa Kijiji Daraja la Tatu

PART A
1. Taja muundo wa Baraza la Madiwani.
Jibu:
-
Madiwani waliochaguliwa kutoka kata.
-
Madiwani wa viti maalum (k.m. wanawake).
-
Mkuu wa Wilaya au Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri – Katibu wa Baraza.
2. a) Taja nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC).
Jibu:
Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi, Sudan Kusini, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).
b) Taja changamoto nne kuu za Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Jibu:
-
Ukosefu wa sera za pamoja.
-
Migogoro ya kibiashara.
-
Tofauti za kisiasa.
-
Changamoto za mipaka na usalama.
3. a) Eleza maana ya maendeleo.
Jibu:
Maendeleo ni mchakato wa kuboresha hali ya kiuchumi, kijamii na kisiasa. Mfano: ujenzi wa shule au hospitali.
b) Eleza maendeleo endelevu.
Jibu:
Ni maendeleo yanayokidhi mahitaji ya sasa bila kuhatarisha mahitaji ya vizazi vijavyo. Mfano: matumizi ya nishati jadidifu kama sola.
c) Eleza uchumi wa kijani.
Jibu:
Ni uchumi unaolinda mazingira na kutumia rasilimali kwa uendelevu. Mfano: kilimo cha umwagiliaji kinachotumia maji kidogo.
4. Eleza kwa kifupi historia ya Mamlaka za Serikali za Mitaa.
Jibu:
Zilianzishwa baada ya uhuru mwaka 1961. Zilifufuliwa tena mwaka 1982 kupitia mfumo wa ugatuaji wa madaraka ili kurahisisha utoaji wa huduma kwa wananchi.
5. Daftari la mali za kudumu litajumuisha nini?
Jibu:
-
Aina ya mali.
-
Jina la mmiliki.
-
Gharama na tarehe ya kununuliwa.
-
Ongezeko la thamani.
-
Taarifa za mauzo.
-
Kila mali iandikwe katika ukurasa wake.
6. Taja hatua za tahadhari dhidi ya majanga.
Jibu:
-
Kubuni mikakati ya kuzuia majanga.
-
Kuwezesha jamii kutekeleza mikakati hiyo.
7. Eleza njia za kudhibiti mapigano katika jamii.
Jibu:
-
Kuimarisha utawala bora.
-
Kukuza uelewa wa utawala bora.
-
Kuwezesha ushirikiano kati ya jamii na viongozi.
8. Ni mambo gani ya kuzingatia ili kikao kiwe halali?
Jibu:
-
Mahudhurio.
-
Mwenyekiti na katibu.
-
Idadi ya wajumbe.
-
Ajenda na muhtasari.
9. Utahakikishaje taarifa za makusanyo ya fedha kijijini ni sahihi?
Jibu:
-
Kutunza daftari la malipo.
-
Kutumia stakabadhi halali.
-
Kudhibiti matumizi kwa nyaraka rasmi.
10. Eleza jinsi utakavyosimamia matumizi bora ya rasilimali za umma.
Jibu:
-
Kupanga matumizi.
-
Kuweka wasimamizi.
-
Kuunda vikundi vya usimamizi.
-
Kutumia mawasiliano na njia za udhibiti.
11. Taja hatua tano za kupambana na umaskini kijijini.
Jibu:
-
Kuelewa hali ya umaskini.
-
Kuainisha sababu.
-
Kuelimisha wananchi.
-
Kutoa mwongozo wa fursa zilizopo.
-
Kuunda vikundi vya uzalishaji.
12. Eleza namna ya kutekeleza kanuni za kilimo bora.
Jibu:
-
Kuandaa mashamba mapema.
-
Kupanda kwa wakati.
-
Kuchagua mbegu bora.
-
Kuhifadhi mazao vizuri.
13. Taja mambo makuu ya kimuungano kati ya Tanzania Bara na Visiwani.
Jibu:
Mambo ni pamoja na:
-
Katiba ya Muungano
-
Ulinzi, Usalama, Uraia
-
Kodi, Elimu ya Juu
-
Sarafu, Bandari, Polisi
-
Mambo ya nje, Mahakama ya Rufaa, n.k.
14. Taja viashiria vitano vya umaskini.
Jibu:
-
Kukosa chakula, elimu, huduma za afya.
-
Ukosefu wa maji safi.
-
Vifo vingi.
-
Kipato duni.
-
Uchakavu wa mazingira.
15. Unapotunza nyaraka za serikali, ni nini cha kuzingatia?
Jibu:
-
Kuhakiki.
-
Kuchambua.
-
Kupanga.
-
Kutunza katika majalada rasmi.
16. Taja majukumu ya mkutano mkuu wa kijiji.
Jibu:
-
Kupokea taarifa za mapato na matumizi.
-
Kujadili mipango ya maendeleo.
-
Kuwachagua viongozi wa kijiji.
-
Kuthibitisha sheria ndogo.
17. Taja misingi ya utawala bora.
Jibu:
-
Utawala wa sheria.
-
Demokrasia.
-
Uwajibikaji.
-
Uwazi.
-
Ufanisi.
18. Taja vyanzo vitano vya mapato ya halmashauri.
Jibu:
-
Mapato ya ndani.
-
Michango ya jamii.
-
Mikopo.
-
Wafadhili.
-
Ruzuku kutoka serikali kuu.
19. Taja alama muhimu za Taifa.
Jibu:
-
Bendera ya Taifa.
-
Nembo ya Taifa.
-
Mwenge wa Uhuru.
-
Fedha ya Taifa.
-
Wimbo wa Taifa.
20. Taja maadili ya utumishi wa umma.
Jibu:
-
Uadilifu.
-
Kutotoa rushwa.
-
Kufanya kazi kwa bidii.
-
Uwajibikaji.
-
Kutunza siri za serikali.
21. Taja rangi za bendera ya Tanzania na maana zake.
Jibu:
-
Nyeusi – watu wa Afrika.
-
Kijani – mimea.
-
Njano – madini.
-
Bluu – bahari, mito na maziwa.
22. Taja majukumu ya Afisa Mtendaji wa Kijiji.
Jibu:
-
Kusimamia mipango ya maendeleo.
-
Kusimamia mapato na matumizi.
-
Katibu wa halmashauri ya kijiji.
-
Kuongoza timu za kiutendaji.
-
Kuhamasisha wananchi dhidi ya njaa na umaskini.
23. Eleza maana ya kamati ya maendeleo ya kijiji.
Jibu:
Ni kamati inayoundwa kwa ajili ya kupanga, kusimamia na kutathmini shughuli zote za maendeleo ya kijiji kwa kushirikisha wananchi.
24. Taja hatua za maandalizi ya kikao cha kijiji.
Jibu:
-
Kutayarisha ajenda ya kikao.
-
Kutoa taarifa ya wito wa kikao kwa wanakijiji.
-
Kuhakikisha mahali pa kikao panafaa.
-
Kuandaa vifaa muhimu (vitabu, kalamu, n.k.).
-
Kuwasiliana na viongozi husika.
25. Kwa nini ni muhimu kuandaa taarifa ya mapato na matumizi?
Jibu:
-
Kuhakikisha uwazi kwa wananchi.
-
Kurahisisha ufuatiliaji wa matumizi ya fedha.
-
Kuwapa viongozi taarifa ya hali halisi ya kifedha.
-
Kusaidia katika kupanga bajeti ya baadaye.
PART B
1. Muundo wa Baraza la Madiwani
Swali: Taja muundo wa Baraza la Madiwani katika ngazi za Halmashauri.
Jibu:
-
Madiwani walioteuliwa kupitia uchaguzi wa kata.
-
Madiwani wa viti maalum kutoka vikundi kama wanawake.
-
Mkuu wa Wilaya au Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ambaye ni Katibu wa Baraza.
2. Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC)
a) Nchi Wanachama:
-
Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi, Sudan Kusini, DRC.
b) Changamoto Kuu:
-
Ukosefu wa sera za pamoja.
-
Migogoro ya kibiashara.
-
Tofauti za kisiasa.
-
Mipaka na usalama.
3. Maana ya Mifumo ya Maendeleo
a) Maendeleo: Mabadiliko chanya katika nyanja za kiuchumi, kijamii na kisiasa. Mfano: Ujenzi wa shule.
b) Maendeleo Endelevu: Maendeleo yanayolinda mahitaji ya vizazi vijavyo. Mfano: Matumizi ya nishati ya jua.
c) Uchumi wa Kijani: Shughuli za uchumi zinazotunza mazingira. Mfano: Kilimo cha umwagiliaji wa maji kidogo.
4. Historia ya Mamlaka za Serikali za Mitaa
Zilianza rasmi baada ya uhuru 1961. Zilirejeshwa tena mwaka 1982 kwa lengo la kupeleka madaraka karibu na wananchi na kurahisisha utoaji wa huduma.
5. Majukumu ya Afisa Mtendaji wa Kijiji
-
Mshauri wa serikali ya kijiji na kamati zake.
-
Msimamizi wa mapato na matumizi.
-
Mlinzi wa amani na utawala bora.
-
Katibu wa Halmashauri ya kijiji.
-
Kutafsiri na kusimamia sheria ndogo.
-
Kuwasilisha taarifa kwa Mtendaji wa Kata.
6. Aina za Migogoro Kijijini
-
Migogoro ya koo.
-
Migogoro ya kaya.
-
Wananchi vs Wawekezaji.
-
Wakulima na Wafugaji.
-
Serikali ya kijiji na taasisi za fedha.
7. Utunzaji wa Mali za Kudumu
Daftari litajumuisha:
-
Aina ya mali, hati na eneo ilipo.
-
Jina la mmiliki.
-
Gharama.
-
Tarehe ya ununuzi.
-
Ongezeko la thamani.
-
Mauzo na taarifa nyingine.
8. Tahadhari dhidi ya Majanga
-
Kubuni mikakati ya kuzuia majanga.
-
Kuwezesha jamii kutekeleza mikakati hiyo.
9. Njia za Kudhibiti Mapigano Kijijini
-
Kuimarisha utawala bora.
-
Kuhamasisha ushirikiano na uelewa.
-
Kukuza umoja kati ya jamii na viongozi.
10. Sifa za Kikao Halali
-
Mahudhurio ya kutosha.
-
Uwepo wa mwenyekiti na katibu.
-
Wajumbe wa kutosha.
-
Ajenda wazi na muhtasari.
11. Usimamizi wa Mapato ya Kijiji
-
Kutumia daftari la malipo.
-
Kutoa stakabadhi rasmi.
-
Kutunza nyaraka zote za fedha.
12. Matumizi Bora ya Rasilimali
-
Kupanga matumizi.
-
Kuweka wasimamizi.
-
Kudhibiti matumizi.
-
Mawasiliano sahihi.
13. Hatua za Kupambana na Umaskini
-
Kuainisha hali ya umaskini.
-
Kuelimisha wananchi.
-
Kuunda vikundi vya uzalishaji.
-
Kutumia rasilimali za eneo.
-
Kutoa hamasa na mwongozo wa kimaendeleo.
14. Utekelezaji wa Kilimo Bora
-
Kuandaa mashamba mapema.
-
Kuchagua mbegu bora.
-
Kutunza mazao.
-
Kufanya kilimo rafiki kwa mazingira.
15. Mambo Makuu ya Muungano
-
Katiba ya Muungano.
-
Mambo ya Nchi za Nje.
-
Ulinzi na Usalama.
-
Kodi, Sarafu, Elimu ya Juu, Uraia, n.k.
16. Viashiria vya Umaskini Tanzania
-
Kutokujua kusoma/kuandika.
-
Ukosefu wa maji safi.
-
Vifo vingi.
-
Utapiamlo.
-
Kipato duni.
17. Utunzaji wa Nyaraka Serikalini
-
Kuhakiki, kuchambua na kuzipanga.
-
Kuzitunza kwenye majalada rasmi.
18. Mkutano Mkuu wa Kijiji
-
Kupokea taarifa za utekelezaji.
-
Kujadili bajeti, mapato na matumizi.
-
Kuwachagua viongozi.
-
Kupitisha sheria ndogo.
19. Misingi ya Utawala Bora
-
Utawala wa sheria.
-
Uwajibikaji.
-
Demokrasia.
-
Uwazi na ushirikishwaji.
20. Vyanzo vya Mapato ya Halmashauri
-
Mapato ya ndani.
-
Wafadhili.
-
Mikopo.
-
Ruzuku ya Serikali Kuu.
-
Michango ya jamii.
21. Alama za Taifa
-
Mwenge wa Uhuru.
-
Wimbo wa Taifa.
-
Bendera.
-
Nembo.
-
Sarafu ya Tanzania.
22. Maadili ya Utumishi wa Umma
-
Bidii kazini.
-
Kutotoa upendeleo.
-
Utii wa sheria.
-
Kutoa huduma bora.
-
Uadilifu na uwajibikaji.
23. Rangi za Bendera ya Tanzania na Maana
-
Nyeusi: Watu wa Afrika.
-
Kijani: Mimea.
-
Njano: Madini.
-
Bluu: Maziwa, mito, bahari.
24. Maana ya Afisa Mtendaji
Mtaalamu aliyeajiriwa kusimamia utendaji wa taasisi au idara.
25. Mabaraza ya Serikali za Mitaa
-
Wilaya: Halmashauri ya Wilaya, Vijiji
-
Mijini: Miji, Manispaa, Majiji
26. Aina za Diwani
-
Walioteuliwa.
-
Waliowekwa na chama.
-
Wabunge wa majimbo.
-
Wanawake walioteuliwa.
27. Bunge ni Nini?
-
Ni chombo cha kutunga sheria.
-
Aina mbili: Bunge la chumba kimoja, vyumba viwili.
28. Umuhimu wa Kudumisha Utamaduni wa Taifa
-
Kukuza maadili.
-
Kulinda rasilimali na mazingira.
-
Kupinga uovu kama dawa za kulevya.
-
Kuinua mshikamano na nidhamu ya kitaifa.
29. Mfumo wa Vyama Vingi (1992)
-
Unalenga uwazi, ushindani wa kisiasa, na utawala bora.
30. Majukumu ya Kamati ya Fedha na Mipango
-
Kusimamia miradi, ardhi, mapato.
-
Kubuni njia mpya za kipato.
31. Sheria Zinazotoa Mamlaka ya Kukamata
-
Sheria Na. 7 ya 1982 (Wilaya).
-
Sheria Na. 8 ya 1982 (Miji).
-
Sheria ya Jinai Na. 9 ya 1985.
-
Sheria ya Mahakimu Na. 2 ya 1984.
32. Sababu za Kusisitiza Maendeleo Vijijini
-
Kilimo ni uti wa mgongo.
-
Ukosefu wa huduma za msingi.
-
Kipato duni na uelewa mdogo wa wananchi.
33. Misingi ya Demokrasia
-
Ushiriki wa wananchi.
-
Uhuru wa maoni.
-
Uchaguzi huru na haki.
-
Haki za binadamu.
34. Walinzi wa Amani
-
Wakurugenzi wa halmashauri.
-
Maafisa Tarafa.
-
Watendaji wa vijiji/mitaa.
35. Utekelezaji wa Ulinzi Shirikishi
-
Kuanzisha mitandao ya ulinzi.
-
Kuitisha mikutano ya ujirani mwema.
-
Kushirikiana na Jeshi la Polisi.